Shekinah Cyber Academy
Course catalog

Bima Talk: Kinga Mali, Biashara na Elewa Madai Kaulimbiu: Jua Bima Yako, Usisubiri Janga Likufundishe!

Bima Talk ni kozi fupi ya vitendo iliyoundwa kuondoa mkanganyiko, dhana potofu, na urasimu unaowakabili wamiliki wa mali, wafanyabiashara, na umma kwa ujumla kuhusu sekta ya bima. Badala ya nadharia ngumu na vifungu vigumu vya kisheria, kozi hii inakupa mwongozo wa moja kwa moja kuhusu namna ya kulinda rasilimali zako na kuhakikisha unalipwa fidia stahiki bila usumbufu pale janga linapotokea. Katika vipindi 4 vilivyosheheni mifano halisi, utajifunza misingi ya mikataba ya bima, tofauti muhimu ya kisheria kati ya bima ya Third Party na Comprehensive, pamoja na mbinu za kukinga maduka, majengo, na mizigo safarini dhidi ya moto, ajali, na wizi wa kuvunja. Zaidi ya yote, kozi inafichua mchakato halisi wa ufuatiliaji wa madai (claims process), nyaraka muhimu zinazohitajika, na mitego ya kawaida inayofanya madai mengi yakataliwe na makampuni ya bima. Malengo Mahsusi ya Mafunzo (What You Will Learn):Kuelewa lugha na kanuni za mikataba ya bima (premium, excess/deductible, na Utmost Good Faith) bila kuhitaji mwanasheria. Kujua haki na mipaka ya bima ya vyombo vya moto ili kutambua nani anastahili fidia chombo kinapopata ajali. Kuchagua bima sahihi ya biashara, stoo, na mizigo ili uwekezaji wako usirudi sifuri baada ya maafa. Kumudu hatua 5 za kufuata madai ya fidia na kuepuka makosa yanayopoteza haki yako ya kulipwa. Walengwa Wakuu (Target Audience):Wafanyabiashara, wamiliki wa maduka, gereji, na maghala. Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto (magari binafsi, malori, na pikipiki). Wasimamizi wa miradi, wasafirishaji wa mizigo, na wananchi wanaotaka kufanya maamuzi sahihi ya kifedha.

TSh pricing Mobile money SMS reminders Verified certificates

0 courses

No courses match those filters

Try a broader search, or clear the filters to see everything.